Saturday, September 11, 2010

Alfajiri na Mapema ndani ya Serengeti NP

mchakato wa kufanya Balloon safari ndani ya hifadhi ya Serengeti huanza alfajiri na mapema ambapo mgeni hufuatwa hotelini kwake na magari ya kampuni ya Serengeti Ballon safari na kuanza safari ya kuelekea eneo ambako safari huanzia. Kutokana na umbali kati ya maeneo zilipo hoteli na eneo la kurukia balloon, safari za wageni kuchukuliwa mahotelini huanzia alfajiri. timu ya tembeatz ilifuatwa hoteli na kuanza safari saa kumi na nusu usiku.

Safari toka Hotelini mpaka eneo la kuanzia safari ya balloon ilichukua takriban saa moja. kwa wengine muda huzidi huo hivyo hufuatwa mapema zaidi. Mchakato wa kuelekea panapoanzia safari za balloon hutoa fursa kwa wageni kufanya safari ndani ya hifadhi usiku (night game drive). Kampuni ya Serengeti balloon safaris ina kibali cha kufanya safari ndani ya hifadhi mida ya usiku. Kutokana na ukweli ya kwamba safari ya gari ilikuwa na lengo la kuwahi kufika eneo la kurukia, njiani hatukuwa na nafasi ya kutafuta au kufuatilia wanyama. tulibahatika kuona viboko kadhaa, fisi 2 na makundi kadhaa ya swala.

Kunapoanza kuchwa, mandhari hubadilika baada ya jua kuanza kuonekana kwa kuvizia. Machweo huwa na msisimko lakini msisimko huu hupata uhondo zaidi unapoushuhudia ukiwa porini huku milio ya ndege na wanyama pori ikiamsha hisia zako za usikivu toka usingizini.

hapo juu likiendelea kushika nafasi yake na kuubadili usiku kuwa asubuhi na kisha mchana. picha zote zilipigwa kabla ya safari ya balloon kuanza. muda huu wafanyakazi huwa wa kampuni ya ballon huwa wanakuwa wanaanda ballon tayari kwa safari.

Picha zote hizi zilipigwa eneo lijulikanalo kama Maasai Kopjes ambako ndio balloons safaris za Serengeti zinapoanzia safari zake ktk hifadhi ya taifa ya Serengeti. Dondoo ambazo tembeatz imezipata ni kwamba hivi sasa balloon safaris zimeanza ndani ya hifadhi ya taifa ya Tarangire. Hii itatoa fursa kwa wakazi wa Arusha na maeneo jirani kufanya balloon safari kutokana na ukaribu uliopo kati ya hifadhi ya Tarangire na Jiji la Arusha na Moshi. tembeaTz bado inazifanyia kazi dondoo hizi na itakupasha habari muda si mrefu baada ya kujua mpango mzima wa huko Tarangire upoje. Stay tuned......

balloon za hifadhi ya taifa ya Serengeti zinasimamiwa na Serengeti balloon safaris nenda sehemu ya Itinerary kupata info za mpango wa huko Serengeti

2 comments:

  1. Kulaleki walahi. Uuuuwi, hizi picha, aaaah! Kwisha kabisa suuzika mwili, nafsi na roho. Nazipenda sana picha za mawio na machweo ya jua, sijui kama iko siku nitaacha kusema hili kila nizionapo. So serene!
    Asante sana KK.

    ReplyDelete
  2. Picha za Sunrise na sunset zinanisuuza roho sana.
    Ahsante sana kwa taswira bomba

    ReplyDelete