
Wengi tumezoea kuiita sehemu hii kama Olduvai (ikiwa na v) lakini ukweli ni kwamba jina au neno stahili la eneo hili ni Oldupai (ikiwa na p). mkanganyiko huu unatokana na wale wataalam waliofika eneo hili awali kuchanganya p na v kutokana na lugha za mataifa yao. Oldupai ni neno la kimasai lenye kumaanisha mmea wa katani mwitu. Mmea ambao umeshamiri sana ktk maeneo haya. Baada ya kugundua masalia haya, wataalam hao walihitaji jina la kulipa eneo (site name) husika kama taratibu zao zinavyoeleza. walipoomba msaada kwa wenyeji (Wamaasai), walipewa jina la Oldupai. Aliyekuwa anaandika notes wakati wa majadiliano hayo akaandika Olduvai badala ya Oldupai.
Eneo hili lipo ndani ye eneo la Ngorongoro conservation Area (NCAA) japo lenyewe lipo nje kabisa ya crater njiani kuelekea hifadhi ya taifa ya Serengeti. Ukiwa unatoka Ngorongoro kuelekea Serengeti kwa gari, Oldupai gorge ipo upande wa kulia wa barabara. Picha toka ktk maktaba ya TembeaTz; unaweza pata dondoo zaidi kwa kubofya hapa
Jambo la Nyongeza:
ReplyDeleteHicho kichuguu unachokiona ktk picha hutumika kama ushahidi kuonyesha matabaka ya udongo yenye kuonyesha matukio mbalimbali ambayo yaliyotekea miaka ya nyuma ikiwemo Volcano za Ngorongoro ambazo zinaelezwa kuwa chachu ya Serengeti kuwa uwanda wa Nyasi kama ilivyo leo. Ni sehemu nzuri ya kujifunza (tena kwa kuona) mambo ya kale
Kk