Saturday, July 3, 2010

ni mtego wa mbung'o

Kitambaa unachokiona kikining'inia ktk mti hutumiwa na wahifadhi ktk mapambano yao dhidi ya Mbung'o. Mbung'o wanapokuwa wengi hushambulia wanyama na kuwaletea magonjwa. ili kuhakikisha kuwa idadi ya mbung'o haifikii kiwango cha kuwa kero kwa wanyama pori na wageni, wahifadhi huwa wanatumia nyenzo kama uionayo ktk hiyo taswira kupunguza idadi yao ktk eneo la hifadhi.
Watafiti waligundua kuwa mbung'o huona kwa urahisi rangi nyeusi na bluu. Kwa kutambua hilo, waliamua kutengeneza mtego kwa kutumia rangi hizo. Vitambaa vyenye rangi nyeusi na bluu huwekwa dawa/sumu ambayo mbung'o akikutana nayo tu basi ndio inakuwa ni tamati yake.

Ukiachia ukweli ya kwamba mbung'o ni kero, kuna upande wa pili wa shilingi wa uwepo Mbung'o ambao una faidia zake. nilidokezwa ya kwamba uwepo wa mbung'o wengi ktk maeneo ya hifadhi yalipekea jamii za wafugaji na hata wakulima kuyakimbia maeneo hayo na kwenda kuishi mbali na maeneo hayo yenye mbung'o (sasa ni Hifadhi). hali hii ilitoa fursa kwa wanyama pori kujinafasi ktk maeneo yenye mbung'o kwa kuwa binadamu alihamishia makazi na shughuli zake mbali na hapo. Moja ya hifadhi ambayo inaelezwa kunufaika na hali hii ni Tarangire ambapo jamii ya wamasai walikimbilia kusini mwa hifadhi kutokana na wingi wa Mbung'o upande wa kaskazini wa hifadhi hii.

1 comment:

  1. Asante KK,
    Nimejifunza jambo jingine leo. Asante kwa elimu!

    ReplyDelete