Tuesday, July 20, 2010

Ni mapito ya wanyama wakienda kunywa maji

Uzionazo sio njia za kuelekea sokoni bali ni njia zinazotumiwa na wanyama ndani ya hifadhi ya tarangire kuelekea ktk moja ya mabwawa ya maji yaliyopo ndani ya hifadhi.

Unavyoenda mbali na bwawa la maji ndivyo njia zinavyozidi kuachana huku kila moja ikishika uelekeo wake. kwa hapa bwawa la maji lilikuwa nyuma yangu.

Kwa wanaotoka kunywa maji wanajua njia za kufuata kurudi walipotoka wafikapo njia panda. wale wanaokuja toka maeneo mengine wanajua njia ya kuifuata kuelekea yalipo maji. Picha hizi zilipigwa wakati wa Walking safari ndani ya hifadhi ya taifa ya Tarangire.

No comments:

Post a Comment