Thursday, June 10, 2010

walikuwa wametoka kuua Swala paa

tuliwakuta hawa Sharubu pembezoni mwa moja ya maziwa yaliyomo ndani ya pori la akiba la Selous wakiwa wamemaliza kumla swala paa. Kuna wageni wenzetu wao ndio walibahatika kuona windo hilo kuanzia walipokuwa wanajipanga kumkamata swala huyo mpaka walipomtia kimiani na kumla. Tulikutana nao njiani ndio wakatupa neno kuwa kuna Sharubu mahali hapo wameangusha swala. tukabadili mwelekeo na kufuata maelekezo yao

Lilikuwa ni kundi la sharubu wasiopungua watano. Waliokuwa wanaonekana kirahisi zaidi walikuwa ni majike watatu huku Sharubu wengine wanaoweza kufikia idadi ya wawili walikuwa wamepumzika ktk mti uliokuwa umejificha na kichaka.

Tulielezwa na wenzetu walioshuhudia tukio hili kuwa swala huyo alikimbilia kwenye tope akidhani kuwa sharubu wangeachana nae. Lakini jamaa walikomaa nae na kumkatia huko huko kwenye matope. Baada ya kuona kuwa wamemaliza kazi ya awali (kuua), walimtoa swala wao ktk tope na kumleta sehemu kavu na kuanza zoezi la kula. ndio maana Sharubu wote unaowaona wamechafuka na matope, ni kutokana na klinyang'anyiro hicho.

Sharubu ni wanyama ambao huyakwepa maji kwa kiasi kikubwa, lakini njaa inapowakatmaa hukimbiza hata kile kinachoelekea kwenye maji.

jamaa wa mizoga nao walikuwepo. Hapo walipo ndipo kulipokuwa na mabaki ya swala waliyemla sharubu hawa. jamaa walishafisha kila kitu wakati sisi tunafika eneo la tukio.
Ni Jambo la kawaida sana muwapo porini na kukutana na kundi lingine na madereva kuanza kuulizana kuuna nini kila mmoja anapotoka. Dereva/guide wenu atamueleza mwenzake kaona nini na wapi na mwenzie atafanya vivyo hivyo. Zaidi ya hapo madereva pia huulizana wapo mnyama fulani ameonekana siku hiyo. Kama mmoja ana fununu yoyote basi atamweleza mwenzie. Madereva wanaopeleka wageni porini wanakuwa na ushirikiano mkubwa sana ktk kutimiza malengo na mategemeo ya wageni wao. Hili naliona ni jambo la Kizalendo sana na tembeatz inawapongeza na kuwasihi muendelee na moyo huo huo.

Ushirikiano huu pia upo hata kwa kutumia teknolojia za kisasa. Dereva akiwa na gari yenye radio call akiona kitu kizuru huwasha radio yake na kufanya broadcast kwa madereva wenzie ambao wana radio zilizo tune ktk masafa yake waweze kufahamu. Hii ya matumizi ya radio call niliishuhudia Serengeti ambapo tuliweza kumuona wajuu baada ya kupata ujumbe kupitia radio call ya gari tuliokuwamo.

No comments:

Post a Comment