Friday, June 11, 2010

Mikoko ya Jozani National park, Zanzibar

Hii ni miti ya mikoko iliyoshamiri ndani ya Hifadhi ya Jozani iliyopo huko visiwani Zanzibar (Unguja). Jozani ndio National park pekee visiwani humo.

Mikoko huota sehemu ambayo kuna maji. Ili kumwezesha mgeni kuweza kuikagua na kuiona miti hii kwa karibu, wahusika wamejenga huu mfumo wa barabara za mbao ambazo mgeni anakuwa anatembea na kujionea hali ilivyo ndani ya hifadhi hii. Ni sehemu nzuri kuitembelea unapokuwa huko visiwani. Unaweza kubofya hapa kujua zaidi kuhusu Jozani. Ahsante ya picha kwa mdau JSK aliyekuwa huko visiwani siku chache zilizopita.

No comments:

Post a Comment