Monday, June 28, 2010

Matete picnic site - Tarangire NP

Ni Sehemu maarufu kwa wanaoitembelea hifadhi ya taifa ya Tarangire. Wengi huja hapa kupata chakula cha mchana wakiwa ktk mizunguko yao ndani ya hifadhi hii. ilitubidi tusubiri kwa muda ili kuweza kupata bench murua lenye uwezo wa kuchukua kikosi chetu chote na kula chakula kwa raha mustarehe. Wageni walikuwa wengi siku hii. Maana vuguvugu la kuanza kwa msimu wa utalii linaonekana wazi.

Usione pako patupu, wakati tunafika hapa tulihangaika kupata sehemu ya kukaa na kula lunch yetu. Tulipotinga hapa ubao ulikuwa umeshika hatamu hata kamera sikuikumbuka. baada ya kula na kushiba ndio nikakumbuka kamera. muda huu (wakati napiga picha hizi) wageni wengi walikuwa wameshaondoka na kuendelea na ratiba zao ndani ya Hifadhi.

Sehemu za kukaa na kupata msosi huku sehemu ya adam na hawa ikionekana kwa nyuma

ukiwa matete unapata view nzuri sana ya mto Tarangire unavyo-flow kwenye bonde. matete picnic site ipo kwenye ukingo wa mlima ambao kwa chini ndio unauona mto Tarangire.

No comments:

Post a Comment