Saturday, May 15, 2010

Njia za Ngorongoro Crater

Ngorongoro crater kuna njia nyingi ambazo zinaweza kukuingiza ndani ya Ngorongoro crater, kukuzungusha ndani ya crater na kisha kukutoa nje. Jambo moja inabidi ulijue kuhusu mapito yako uwapo ndani ya Ngorongoro crater ni kwamba njia ya kuingilia ndani ya crater (crater descent route) ni tofauti na njia ya kutokea nje ya Crater (crater Ascent route). Picha juu ndio njia ya kuingilia Ngorongoro crater.

Hii ni moja ya njia zilizopo ndani ya crater ambazo zitakuzungusha na kukufikisha kona mbali mbali ndani ya crater. Hii inaelekea bwawa la Ngoitoktok ambako ni picnic point mojawapo ndani ya Ngorongoro crater.

Hii nayo ni moja ya mapito ndani ya Ngorongoro crater. Licha ya kwamba toka juu ngorongoro crater inachukua mfano wa bakuli na kuoneka dogo lakini ukiwa ndani ya Ngorongoro crater ni rahisi sana kupotea kama hujui njia au huelewi wapi pa kwenda. Changamoto ya kwanza huja kutokana na ukweli wa kwamba unapoingilia sipo unapotokea. Njia hizi zipo sehemu mbili tofauti na usipoelewa unaweza tumia muda mwingi kutafuta pa kutokea badala ya kutafuta na kuangalia wanyama na mandhari ya crater. Kuwa na guide au dereva mwenye uelewa wa mapito ya crater ni jambo la msingi na manufaa sana kwa safari yako. Off road driving hairuhusiwi ukiwa ndani ya Ngorongoro crater.

1 comment:

  1. DESCEND..KUSHUKA, KWENDA CHINI , KUTEREMKA.
    ASCEND... KWENDA JUU, KUPANDA, KUPAA.
    LAZIMA TUJIFUNZE KIINGEREZA ILI TUWEZE KUWA NA MAWASILIANO SAHIHI.
    DESCENT NA ASCENT NI MANENO SAHIHI YA KIINGEREZA LAKINI HAPA SI MAHALI PAKE.

    ReplyDelete