Masikio ni jina la 'utani' ambalo huyu mnyama amepewa na wazee wa pori. Nia ya kumpa jina na mengine kwa wanyama wengine ni kumficha mgeni wake asijue anamtafuta mnyama gani anapokutana na dereva mwenzake ndani ya hifadhi. Hii inamfanya mgeni asijue nini atakutana nacho.
Ktk lugha yetu ya kiswahili tuna maneno mengine mawili ambayo yanakuwa yanatumika kumtambulisha masikio. hayo ni Tembo na Ndovu.
Mwenzenu kiswahili nilinusurika 'kusukutua' kidato cha nne nikatokea mlango wa dharura (Msianze sasa...) kwa hiyo sitaki kujivika kilemba cha ukoka! Nakuja kwenu wadau mnisaidie kupata ukweli wa hili. Kuna tofauti yoyote kati ya Ndovu na Tembo? Naomba nielekezwe matumizi sahihi ya haya majina mawili ili niweze kuyatumia ipasavyo. Naomba msaada wenu wadau ambao naamini wengi watanufaika nao pia. Nawasilisha kwenu.
Meno ya Tembo; Pembe za Ndovu
ReplyDeleteDuh! yaani nilikuwa sijawahi kujiuliza hizi tofauti.
Mdau, nilithani unauliza swali ambalo nami linanisumbua. Ni kwamba, utasikia, jangili amekamatwa na meno ya tembo. Hivi kweli ni
ReplyDelete"meno" au "pembe" zake? Naomba kuwakilisha