
Fundi chuma hujenga viota vikubwa na kwa kutumia malighafi mbalimbali ambazo anaweza kuzipata ktk maeneo anayopita. hutumia udongo, miti, mawe madogo madogo na wakati mwingine hata vipande vya mifuko ya plastiki na nylon vimewahi kutwa ktk kiota cha fundi chuma. Ilihali ndege wengine hutumia miti na majani kutengenezea viota vyao.
Jambo moja ambalo lilipita masikioni mwangu ni kwamba, cheza mbali na kiota cha fundi chuma. Inaelezwa ya kwamba (sina ushahidi) ukikiharibu au kubomoa kiota cha fundi chuma (ndege), basi kama ulikuwa una nyumba yako, hiyo nyumba yako ipo hatarani kupotea kwa namna yoyote ile - mafuriko au moto. wapashaji habari walienda mbele na kusema kuwa endapo kama hauna nyumba, basi nafasi ya wewe kuja kuwa na nyumba yako ndio inakuwa imetoweka.
Nilidokezwa ya kwamba hii dhana ipo miongoni mwa makabila mengi ya hapa nchini. Ukweli ni kwamba hii issue ni kama sumu, haionjwi! so ukweli wake inabidi uupate kwa kupitia neno la mdomoni. Mara nyingi fundi chuma huwa na tabia ya kukikacha kiota chake endapo atagundua kuwa hakivutii majike.
picha juu ni kiota cha fundi chuma (hilo fungu unaloliona ktk huo mti) kilichojengwa ktk mti pembezoni mwa Mto Ruaha, ndani ya Ruaha NP. Ahsante ya picha kwa mdau Thom wa Kimasafaris.
mbona hujamalizia sasa?!!
ReplyDelete