Inawezekana mdau umezoea kupanda midege mikubwa Boeing au Airbus lakini haujapata nafasi ya kupanda ndege ndogo (wengine huziita ndege za kukodi). Hii ni Ndege aina ya Cessna 208 Caravan. Hapa wadau tuliokuwa tunafanya nao safari toka Dar kwenda Unguja (Zanzibar) wakianza maandalizi ya safari. Safari ya ndege kati ya Unguja na Dar huchukua takriban dakika 20 (kuruka hadi kutua).
Hizi ndege ni zimekuwa ni nyenzo muhimu sana ktk sekta ya utalii kwa hapa Tanzania. Nchi hii ni kubwa na vivutio vimetapakaa ktk kila kona ya nchi yetu. Ndege hizi zimeku zikitumika sana na wageni ambao hupenda kutumia muda mchache kusafiri na muda mwingi kupumzika au kutembelea vivutio vyetu. Ni ndege ambazo hazina mahitaji makubwa kwa kiwanja. nyingi hufanya safari zake ktk viwanja vilivyotapakaa ktk hifadhi zetu mbali mbali ambavyo navo havina lami na vifaa kama vilivyo viwanja vya kimataifa. ni dhahiri uwepo wa hizi ndege na matumizi yake ktk sekta ya utalii na nyingine nyingi ni jambo linalosaidia maendeleo ktk sekta ya utalii kwa kiasi kikubwa.
No comments:
Post a Comment