Tuesday, January 19, 2010

Sharubu akiwa na wanae


Unapokuwa ktk misele ya porini ndani ya Serengeti National Park, ukiyakaribia mawe yaliyopo huko nenda kwa step kwani unaweza kuona sharubu akiwa anakula timing au kapumzika.

Simba huishi ktk makundi ambayo huongozwa na simba Dume (mmoja au hata wawili). Ndani ya kundi huwa kunakuwa na majike kadhaa. Kundi huwa na himaya (teritory) ambayo ni kazi ya Dume kuhakikisha kuwa hakuna dume mwingine anaeingia ktk kundi lao. Dume hulinda mipaka ya himaya kwa kuweka alama za mikojo (Scent marking) ili kuwahabarisha madume wengine kuwa eneo hilo lina mwenyewe na wao wakae mbale au waende kwengine.
Ktk mgawanyo wao wa kazi, simba jike kazi yao kubwa ni kuwinda ilhali dume kazi yake ni ulinzi sambamba na uzazi akishirikiana na majike.

Hawa jamaa wana utaratibu ambao ki binadamu tunaweza kuuita ni ukatili.
Simba dume huwapanda majike walio ktk eneo lake na kuwapa mimba ambayo baadae huja kuzaa watoto (Simba huzaa zaidi ya mtoto mmoja- kama ilivyo kwa mbwa). Endapo simba dume mwingine ataweza kuvamia teritory ile kwa kumpindua dume (baada ya mapigano makali), basi dume vamizi huuwa watoto wote waliochwa na dume la awali. Hii hufanywa ili kuhakikisha kuwa anaharibu kabisa uzao wa aliyemtangulia.
Cha ajabu ambachi ni kweli kabisa ni kwamba, siku chache tu baada ya watoto kuuliwa na mvamizi, mama zao huingia ktk joto na hivyo kuwa ktk hali tayari ya kubeba ujauzito wa dume vamizi (ambalo ndio litakuwa mtawala kwa muda huo).

Imekaa kikatili lakini ndio jinsi ambayo simba dume anahakikisha kuwa uzao wake pekee ndio unaendelea kushamiri na ule wa mwingine unaangamizwa kwa namna yoyote. maujai haya huwakuta watoto wadodo ambao hawawezi kujitetea.

No comments:

Post a Comment