Hata kama sehemu kubwa ya gari ipo wazi. Unapokuwa ndani ya gari utajihakikishia usalama wako dhidi ya wanyama wakali kama Simba, chui na duma.
Japo si kwa wanyama wote lakini kwa sharubu, wa chini na wajuu. ukiwa ndani ya gari kama hizo, hawatakuletea shida yoyote. endapo utakutana nao ukiwa nje ya gari basi hapo ama zako ama zao.
Japo si kwa wanyama wote lakini kwa sharubu, wa chini na wajuu. ukiwa ndani ya gari kama hizo, hawatakuletea shida yoyote. endapo utakutana nao ukiwa nje ya gari basi hapo ama zako ama zao.
Hii inatoka na saikolojia ya wanyama hawa kwamba wanaona gari kama kitu ambacho hawana faida nacho so hata wewe uliyeopo ndani ya gari unaonekana kama kitu ambacho sio dili kwao. unaposhuka kutoka katika gari na kuwa mwenyewe kwanza hapo unakuwa umejitenga na gari ambalo wao wanaliona halina dili. lazima wataanza kukuthaminisha wewe ili wakuelewe, haitachukua round watagundua kuwa wewe ni dili kwao so watakuwekea mpango wakubane.
Simba huua wanyama kwa kumbana koo mnyama (wengine husema simba anakuwa ananyonya damu, hii si kweli) ili kumkosesha hewa. anapoliangalia gari, anakuwa anashindwa kujua kama akitaka 'kuliua' gari alikabie koo wapi, akikosa jibu anaachana nalo na kuangalia ustaarabu mwingine.
jambo lingine ambalo linakuweka ktk hatari unapokuwa haupo ktk gari ni kwamba unakuwa upo level moja na simba huyo hivyo anakuona unaingia anga zake. Simba ni teritorial (mnyama mwenye kujenga na kulinda himaya yake), hivyo hakubali mnyama mwingine aingie ktk anga zake. atachukua tahadhari madhubuti kulinda himaya yake na ktk tahadhari zake kukumaliza kabisa ni moja ya option alizo nazo ktk madesa yake ya kulinda teritory yake.
kwa Tembo,nyati au kifaru habari inakuwa ni tofauti, wao inabidi ucheze nao kwa step kwani saikolojia yao ipo tofauti na wanyama wanaokula wanyama wenzao - carnivores. ni Vyema hawa watatu usiwakaribie kwa karibu. hawa wanatumia msuli ktk kujitetea when you get too close for comfort.
Nimeipenda hoja ya simba kushindwa kujua "koo" la gari liko wapi ili aweze kulibana.
ReplyDelete