Unapokuwa mapumzikoni kisiwani Unguja, moja ya shughuli unayoweza kuifanya ukiwa huko ni kuzungukia maeneo kadhaa ya kisiwani humo (hasa hasa maeneo ya Kaskazini - Nungwi) kwa kutumia majahazi (dhow safaris). Majahazi yao ni salama na yanakuwa na life jackets ambazo unavaa muda wote wa safari
Raha huongezeka mkiwa wengi, kwani mnakuwa mnashindana. Mwanzoni nilikuwa na dhana ya kwamba haya Majahazi (kwa kuwa yanategemea upepo) basi daima yataenda upande ule tu ambao upepo unaelekea. lakini safari hizi za Majahazi zilinipa picha tofauti.
kwa kugeuza mkao wa tanga (kile kitambaa cheupe kikubwa), nahodha anaweza kubadili mwelekeo na kuelekea kokote kule anakotaka. hili jambo lilinishangaza lakini ndio ikawa kweli ya mambo. Challenge kubwa wanaipata endapo upepo utakuwa hauvumi, haupo. hapo jahazi linaweza simama au kuanza kusukumwa na maji.

No comments:
Post a Comment