Mamba huzaliana kwa kutaga mayai. Muda wa kuyataga mayai ukifika, mamba hutafuta eneo nje ya mto au bwawa ambako ni salama. Huchimba shimo na kisha kutaga mayai. Akimaliza hulifukia shimo vizuri na kulilinda kwa namna yoyote dhidi ya wavamizi na wezi wa mayai (kenge, ngedere na hata binadamu).
Kwa wanyama wengi wanaotaga, jinsia ya mtoto aliyeopo ktk yai huwa inakuwa imeshajulikana pindi yai linapotagwa. kwa mamba hali haipo hivyo.
Jinsia atakayozaliwa nayo mtoto wa mamba anaipata baadae na inachangiwa sana na joto ambalo lilifikia yai alilokuwemo mtoto mamba alipokuwa kichanga. Mayai ambayo yatapata joto la juu kidogo hayo yatatotoa mamba dume. ilihali yale ambayo yatapata joto si jingi sana, basi hayo yote yataishia kutotoa mamba jike.

Ndugu tembea,
ReplyDeleteTueleze ikiwa joto liko la wastani haliko zaid wala haliko kidogo. Je mamba atakaezaliwa atakua ana jinsia mbli?