Monday, January 4, 2010

hata mbuyu huanza kama mchicha

Ukitembelea makumbusho ya Bagamoyo utakuta na huu mnyororo uliochomoza ktk mbuyu. Inaelezwa kuwa huu mnyonyoro ulikuwa ukitumika na Mtawa (sister) kumfungia punda wake anzi hizo za ukoloni. kwa kuwa mbuyu huu unakua, mnyororo unakuwa unamezwa kinamna na mbuyu. yawezekana siku moja kipande hiki cha historia kikamezwa na mbuyu na kutoweka kabisa

kwa mtu ambae ana mwelekeo wa u-Tomaso, vitu kama hivi vinafaa sana kumdhirishia usemi wa kwamba hata mbuyu huanza kama mchicha

1 comment:

  1. Hili suala la mbuyu kuanza kama mchicha linakikumbusha ubishi mkubwa uliotea siku moja nasafiri kwenda Mbeya maeneo ya ruaha mbuyuni. Watu wanahoji Je kuna mibuyu inayoota sasa hivi au ndo imeisha? Je unaweza utambua mbuyu ulioko na ukubwa wa mchicha? Mwingine akadai mbuyu una evolve, ulikuwa mtu flani una transform kuwa mbuyu baada ya umri au ukubwa flani.... Ilikaribia kupaki gari kuusaka mbuyu ulio japo kimo cha kuku kujiridhisha.Mpaka leo sijawahi ona mbuyu ukiwa mdogo ka mchicha may be siujui ukiwa mdogo ndo maana siuoni, its nice fenomenon any way...

    ReplyDelete