kwa wanaokwea mlima kupitia route ya Marangu, shughuli huwa inaanzia hapa. Masaa unayoyaona (ETA) ni masaa ambayo mpandaji anategemewa kuyatumia kutooka point moja kwenda nyingine. kwa mfano wameandika Mandara 3Hrs, hiyo inamaanisha ni muda wa safari toka Marangu gate (hapo ilipopigwa picha) hadi Mandara.
Soma notes vizuri ubaoni ili usije ukafeli mtihani wa kupanda mlima. Ni muhimu sana kuzingatia haya maelekezo kwani ikuyapuuza maisha yako yanaweza kuwa hatarini pia. Huu ni muongozo tu ili kukuwezesha mpandaji kufanikisha lengo lako la kupanda mlima hadi kileleni.
dondoo kuhusu viwalo vya kutinga wakati wa shughuli nzima ya kupanda mlima Kilimanjaro. Kutokuwa na viwalo isiwe kikwazo kwako, Marangu gate kuna wajasiriamali wanakodisha pamba mahususi kwa ajili ya kupandia mlima. Huna haja ya kununua au kusafiri na makoti yako kwa ajili ya kujilinda na baridi wakati wa kupanda mlima.
No comments:
Post a Comment