Baada ya kutokuwepo mjini kwa muda wa siku chache, niliporudi tu nikatua ktk blog ya ankal ili kujua mambo yameendaje mjini.
nilistaajabika kukutana na story ambayo mimi nilikuwa na taswira zinazoelezea hali halisi.
hii ni story ya twiga wa Arusha national park kutokuwa na sehemu ya mwisho ya mkiani ambayo huwa na manyoya. Juu ni taswira za twiga amba tulibahatika kukutana nae ndani ya Arusha park akiwa hana sehemu ya mwisho ya mkia wake. ukiangalia taswira ya pili utaona ni dhahiri mkia wake ni butu mwishoni.
Ndio mambo ya porini, aina fulani ya mnyama anapokosekana ktk pori au mbuga, basi ukosekanaji wake huwa na madhara ya kipekee kwa mazingira na wanyama wengine.
soma story zaidi ktk blog ya Michuzi aka Ankal - http://issamichuzi.blogspot.com/2009/12/twiga-wa-hifadhi-za-arusha-wakosa-mikia.html#comments
No comments:
Post a Comment