Saturday, August 27, 2016

Porini anaitwa Kamba kubwa

African Python Tembea Tanzania Mikumi National Park
Ukiwa porini halafu ukasikia habari ya kwenda mahali kuiona kamba kubwa basi ujue huko muendako mtaenda kuonana na unayemwona kwenye post hii. Ni Chatu. Tulibahatika kumkuta kwenye mti karibu kabisa na Bwawa la viboko ndani ya hifadhi ya taifa Mikumi. Wenyeji wanafahamu kuwa hapo ndio kijiwe chake mida ya mchana. Kusema ukweli hii ilikuwa ni mara yangu ya kwanza maishani mwangu kukutana na chatu akiwa kwenye mazingira yake ya kawaida porini. mara kadhaa nimewaona kwenye maonyesho au wakiwa wamefungiwa kwenye Zoo mbalimbali nilizowahi kuzitembelea.African Python Tembea Tanzania Mikumi National Park
licha ya kuzungukwa na magari kadhaa, aliendelea kuuchapa usingizi wake bila wasiwasi

African Python Tembea Tanzania Mikumi National Park
Kama sio kuwa na wenyeji, tungeweza kumpita bila kubaini uwepo wake kwenye huu mti pembezoni ya barabara. Mwenyeji aliomba gari ipunguze mwendo ili aukague mti vyema. na ndipo tulipoweza kumuona vyema.

No comments:

Post a Comment