TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
OLDUVAI GORGE IKO TANZANIA SI KENYA
Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imekuwa ikifuatilia kwa
makini majadiliano yanayoendelea katika mitandao mbalimbali ya kijamii kufuatia
video iliyotumwa katika YouTube https://www.youtube.com/watch?=iveX49WE7fw
na imekuwa ikisambazwa kupitia njia mbalimbali za habari ikimuonesha mtu mmoja
kutoka nchi jirani akisema kuwa Olduvai Gorge ambayo kimsingi iko Tanzania kwamba
iko Kenya.
Video hii imeibua majadiliano katika mitandao ya
kijamii baina ya watanzania na watu wengine ambao wanaitakia mema Tanzania na
wanaoelewa vizuri kuwa Olduvai Gorge iko Tanzania.
Bodi ya Utalii Tanzania kama taasisi ya Umma yenye
jukumu la kuvitangaza vivutio vyetu vya utalii imeshtushwa na video hii
iliyojaa upotoshwaji mkubwa ambao tunaamini mbali ya malengo mengine inalenga
kuchafua kazi nzuri ambayo imekuwa ikifanywa na Bodi kwa kushirikiana na wadau
wengine katika kutamgaza vivutio vya utalii vya Tanzania ikiwemo Olduvai Gorge.
Tunapenda kuchukua fursa hii kupinga vikali upotoshwaji
huu uliofanywa na mtu huyo wakati akihutubia mkutano amabao tumeambiwa ulikuwa
ni wa Vijana wa Umoja wa Mataifa uliofanyika Amerika mwezi Agosti mwaka jana. Tunapenda
dunia ifahamu kuwa kama ilivyo kwa Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Taifa ya
Serengeti, Zanzibar n.k Olduvai Gorge mahali panapoaminika kuwa ndipo binadamu
wa kwanza duniani aliishi na ambako Dr. Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la
binadamu huyo wa kale anayesadikiwa kuishi miaka takribani milioni 2 iliyopita
iko pia Tanzania na si mahali pengine popote duniani. Eneo hili la Olduvai
Gorge liko katika bonde la ufa katikati ya bonde la Ngorongoro na Hifadhi ya
Taifa ya Serengeti mkoani Manyara nchini Tanzania.
Tunatoa wito kwa watanzania mahali popote walipo
kuendelea kuunga mkono juhudi za Bodi ya Utalii Tanzania za kuitangaza Tanzania
na vivutio vyake vya Utalii kwa kujibu na kusahihisha papo hapo bila woga mara
tu taarifa ya upotoshaji kuhusu nchi yetu inapotolewa iwe ni kwenye mikutano ya
ndani ya nchi au ya Kimataifa. Tunaamini kuwa ni jukumu la kila mtanzania
kuitangaza Tanzania na vivutio vyake vya Utalii badala ya kuiachia TTB kazi hii
peke yake.
Yawezekana katika mkutano huo wa vijana ambao mjumbe
huyo wa nchi jirani alipata fursa ya kuzungumza na kufanya upotoshaji huzo,
wajumbe wa Tanzania pia walikuwepo ambao wangweza kukosoa upotoshaji huo papo
hapo na kuelezea ukweli na usahihi wa mahali ilipo Olduvai Gorge.
Imetolewa na:
Ofisi
ya Uhusiano
BODI YA UTALII TANZANIA
No comments:
Post a Comment