Mdau Samson ambae yupo Ruaha NP amenitumia picha hii muda mfupi uliopita ikimuonyesha Chui aka Wa Juu akawa kwenye mizunguko yake ya asubuhi. Chui ni mmoja wa wanyama ambae ni nadra sana kuonekana na huwa anaonekana aidha asubuhi na mapema au jioni. Ni mnyama ambae hupenda kufanya mawindo na matembezi yake mida ya usiku. Hutumia muda wa mchana kupumzika na mara nyingi hupenda kupumzika juu ya miti. ndio maana wazee wa pori wakampa jina la "wa juu". kwa kukaa juu ya miti mikubwa huweza kukwepa usumbufu wa wanyama wengine kama fisi, simba na wengineo ambao wanaweza wakamshambulia akiwa usingizi/
Bro KK,
ReplyDeleteI Just heard that this creature sleeps 22 hours in a day!!! Is it true?