Saturday, August 2, 2014

A glimpse of the Nungwi Coast from a Boat Ride - Nungwi Coast, Zanzibar

Nungwi Coast Zanzibar
Hizi picha nilizipiga mwezi April, huko Nungwi nikiwa kwenye boti. Majengo yanayoonekana ufukweni karibia yote ni majengo ya hoteli mbalimbali zilizopo kwenye pwani ya eneo hili. Ni hoteli nyingi na ni kivutio kikubwa kwa watalii wanaopenda mapumziko ya sehemu za pwani na michezo ya Baharini. Kwa wageni wengi wanaokuja kutembelea Hifadhi za huku Bara, hupendelea kumalizia safari zao kwa mapumziko mafupi kwenye hoteli hizi kabla ya kupanda ndege na kurudi makwao. Kama wewe umeshawahi kukanyaga pande za Nungwi, basi unaweza ukazitambua baadhi ya hoteli zinazoonekana kwenye picha zilizopo kwenye post hii. 

Nungwi Coast Zanzibar
Ndugu zetu wa Zanzibar wamejitahidi sana kuzitumia pwani zao kwa shughuli za kiuchumi hususan mahoteli ambayo yanatoa ajira za moja kwa moja kwa wananchi wengi - Wa Visiwani, wa kutoka huku Bara na hata wa kutoka mataifa mengine ya Afrika na kwengineko. Nungwi ndio eneo lenye mkusanyiko wa Hoteli nyingi za kitalii  kisiwani Unguja. Hoteli nyingine zipo ukanda wa Pwani Mchangani na kwengineko, upande wa Mashariki wa kisiwa cha Unguja.


Nungwi Coast Zanzibar

Nungwi Coast Zanzibar

Nungwi Coast Zanzibar

1 comment: