Monday, March 31, 2014

Conde Nast Traveller Magazine; Migahawa 10 iliyopo kwenye sehemu usizozitegemea, Namba 4 imetoka Zanzibar

The Rock Restaurant Zanzibar
Ni Orodha ya Migahawa kumi iliyopo kwenye sehemu usizozitegemea iliyotolewa na Jarida la Conde Nast Traveller, umeiweka mgahawa wa Rock Restaurant uliopo visiwani Zanzibar kwenye nafasi ya nne dhidi ya migahawa mingine kumi ambayo ipo sehemu usizozitegemea . The Rock Restaurant ndio mgahwa pekee kutoka Africa uliochomoza kwenye orodha hii na kuweza kushika nafasia ya nne. Migahawa mingine imetoka sehemu mbalimbali za Duniani kama vile Marekani, Maldives, Italia na kwengineko.  Bofya hapa kuona orodha yote ya jarida la Conde Nast Traveller


The Rock Restaurant Zanzibar
Mgahawa wa The Rock Zanzibar upo kwenye pwani ya Kusini Mashariki mwa kisiwa cha Unguja na Mgahawa huu ulianzishwa mwezi Julai 2010. Ni moja ya sehemu za Zanzibar ambazo zimepata kutawala mitandao ya kijamii na nyanja nyingine za mawasiliano mtandao.

The Rock Restaurant Zanzibar

1 comment:

  1. Nimeipenda sana hii. Congratulation to the master mind behind this creativity.

    ReplyDelete