Sunday, February 2, 2014

Adobe haihusiki kabisa hapo, Ni tukio la kweli..

Hakuna kuchakachua kwa namna yoyote ile kwenye picha hii, kwa wazee wa pori hili ni moja ya matukio nadra ambayo dereva na mgeni huyaota. Chui au Duma huwa na tabia ya kupanda kwenye bonet za magari na kukaa kwa muda kidogo. Hii huchangiwa na mazingira waliopo ambapo hulitumia gari kama kichuguu kwa lengo la kuweza kuona mbali au wakati mwingine hata kupata joto la engine ya gari hususan vipindi vya baridi kali huko maporini. Tukio hili lilitokea huko Serengeti aka Shambani ambako wa Juu (Chui) huyu alipanda juu ya bonet ya hii gari na kukaa hapo kwa muda wa kama dakika 5 na baadae kushuka na kuendelea na hamsini zake. Kwa hofu, wageni waliamua kuchukua tahadhari mapema ya kufunga roof ya gari yao. Kwa wazoefu, Roof hubaki wazi na mnyama haleti madhara yoyote.
Shukran ya picha Mdau Assery wa Arusha

3 comments:

 1. Super great shot. The Serengeti. The great Tanzania

  Muro

  ReplyDelete
 2. Super great shot. The Serengeti. The great Tanzania

  Muro

  ReplyDelete
 3. what? that is more than an adventure.

  ReplyDelete