Saturday, January 18, 2014

Mikumi National Park leo hii - 18th Jan

Mdau Thomas wa HSK SAFARIS yupo Mikumi NP muda huu na hizi ni picha kadhaa alizoturushia.
Kama umepata fursa ya kuona ile video ya kule bondeni(+27) ambako tembo aligalagaza VW, basi utaelewa ni kwanini hapa Mdau Thom aliwapa right of way hawa jamaa.Kuna wakati Mvua ilikuwa ikinyesha lakini game drive iliendelea kama kawa. Kwa hifadhi ya Mikumi mvua sio tatizo sana kwani barabara zake ni nzuri na nimedokezwa kuwa zilipigwa sop-sop pale ambapo kulikuwa na mategemeo ya kuwa Mkuu wa +1 angeweza kwenda huko alipokuja nchini mwaka jana. Ratiba ambayo ilikuja kubadilishwa baadae. Japo hakwenda lakini maandalizi yake yalipelekea maboresho ya barabara za ndani za hifadhi yetu

Shukran ya Picha Mdau Thomas wa HSK Safaris

No comments:

Post a Comment