Saturday, October 5, 2013

Lion Kill.. Ngorongoro Crater

 Mdau Thomas alibahatika kumuona huyu Sharubu aliyekuwa amejificha chini ya mti akiendelea kula windo lake la pundamilia. Simba huwa na tabia ya kuficha mawindo yao kwenye vichaka kama hivi ili kuweza kuwakwepa Tumbusi wasibaini windo lake na kumletea zengwe wakati akila. Anapojificha chini ya mti au kichaka namna hii huwa na fursa ya kuweza kula kwa nafasi japo wakati mwingine wazengeaji wa ardhini kama bwana Afya huweza kumletea zengwe pia. Mnapokuwa porini, wazee wa pori huwatumia ndege aina ya Tumbusi ili kuweza kubaini kama eneo fulani kuna windo la Sharubu, Wa Chini au Wajuu.. Wanapoonekana kuruka wengi angani huku mmoja baada ya mwingine akiwa anaelekea kutua ardhini basi ni dhahiri eneo hilo kunakuwa na jambo zuri la kulifuatilia na kujionea



Sharubu = Simba
Wa Juu = Chui
Wa Chini = Duma
Shukran ya picha kwa Mdau Thomas wa HSK Safaris

No comments:

Post a Comment