Dar es Salaam. Sekta za usafiri wa anga na utalii zinakabiliwa na upungufu mkubwa wa wataalamu hali iliyosababisha Tanzania kukosa watalii wa kutosha, Hatua hiyo imezilazimu baadhi ya kampuni za usafiri wa anga na utalii kwenda vyuo vikuu ili kuwaomba wahitimu kuja kujiunga na sekta hizo. Akizungumza jana wakati wa kusherehekea miaka 15 ya Kampuni ya Travelport inayosambaza mfumo unaotumika kukata tiketi za ndege kwa njia ya mtandao, Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Eliasafi Mathew, alisema hivi sasa wameanza kwenda vyuo vikuu kuwaomba wahitimu. Alisema walishakutana na uongozi wa Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS) na kwamba shule hiyo imeanza kufundisha baadhi ya kozi zinazohusu sekta hizo ili kukabiliana na upungufu huo.
Chanzo; Mwananchi
No comments:
Post a Comment