Tuesday, July 16, 2013

Pilikapilika kwenye geti la Machame leo asubuhi

Ni Geti la kupandia mlima Kilimanjaro kwa njia ya Machame. Picha hizi zimepigwa leo asubuhi hapo getini na Mdau Aenea wa Tanzania Girrafe safaris alikuwa amesindikiza wageni wake kuanza safari ya kuupanda mlima kilimanjaro kwa muda wa siku 7. Hapo kila mmoja ana jukumu lake na kila mtu akiwa anawajibika illi mgeni wake aweze kufurahia safari yake ya mlima. Mizigo ni mingi kwa sababu wanaopanda Mlima Kilimanjaro kwa njia ya Machame wanalala kwenye mahema, tofauti na wale wa Njia ya Marangu. Huku karibu kila kitu inabidi kibebwa na wasaidizi aka wagumu.

Mdau Aenea Kushoto akiwa na wageni wake aliowasindikiza leo asubuhi kwenye geti la Machame kuanza safari yao ya kuupanda Mlima Kilimanjaro

High season imechanganya Mlimani

No comments:

Post a Comment