Monday, April 15, 2013

Mabanda wanamolala wanaopanda Mlima Kilimanjaro kwa njia ya Marangu

 Haya ndio mabanda wanamolala wageni wanaopanda mlima Kilimanjaro kwa njia ya Marangu. ifahamike ya kwamba, ni njia ya Marangu pekee (kwa mlima Kilimanjaro) ambapo mgeni anakuwa na fursa ya kulala kwenye banda. (Huts). Wapandaji wa njia nyingine wanalala kwenye mahema madogo au makubwa. Picha juu ni moja ya mabanda yaliyopo kwenye kituo cha Mandara. Banda hili limegawanywa sehemu mbili ambako kila sehemu ina uweze wa kulaza wageni wanne. Mabanda yana solar hivyo wageni wanakuwa na uhakika wa mwanga japo ukitaka kuchaji simu au kamera inabidi uende kwenye banda la wasimamizi ambako wao ndio wana socket. Vyumbani kuna switch ya taa na taa yenyewe tu. Kwa anayepanda kwa njia ya Marangu, atalala kwenye huts kama hizi katika kituo cha Mandara na Horombo. Kituo cha Kibo kina chumba kilichojengwa kwa mfumo wa bweni lenye vyumba kadhaa ndani yake. Lipo tofauti kidogo na hizi huts za Mandara na Horombo.

Hali ilivyo ndani, hii ni sehemu ya upande mmoja wapo wa banda tulilolala sisi. upande wa pili kuna sehemu nyingine yenye uwezo wa kulaza wageni wanne. mpango ulivyo ndani ni wageni watatu wanalala kwenye hivi vitanda vya chini wakati mmoja analala hapo juu. Magodoro unayakuta ktk hut isipokuwa mgeni unalala kwenye sleeping bag yako uliyokuja nayo.


No comments:

Post a Comment