Saturday, April 13, 2013

Kutoka Marangu Gate Mpaka Mandara Hut

Marangu gate to Mandara hut
Hili bwawa lipo mwanzoni kabisa wa safari baada tu ya kuvuka eneo la mwisho la ukaguzi kwenye geti la Marangu. Ni bwawa linalotengenezwa na moja ya mito inayotiririsha maji toka Mlimani. hapo unavuka kwa daraja - eneo ambalo mpiga picha hii alikuwa kasimama.

Marangu gate to Mandara hut
Safari ikiendelea, Mimi kushoto na Guide wetu aliyejulikana kwa jina la Erigard (kulia)

Marangu gate to Mandara hut
Hili ndio Daraja la kwanza kuvuka baada ya kuanza safari. Mdau Frank akiwa amepozi juu

Marangu gate to Mandara hut

Marangu gate to Mandara hut

Marangu gate to Mandara hut

Marangu gate to Mandara hut
Mapumziko ruksa hasa pale mwili unapohitaji kupumzika. japo ni ngwe ya kwanza ya safari lakini tulilazimika kuweka vituo kadhaa ili kupumzisha mwili na kunywa maji. Licha ya hali nzuri ya hewa safi na kabaridi kwa mbali, Kiu inakubana kama upo kwenye joto la pwani. Maji ni muhimu sana kwa mpandaji na unatakiwa uwe nayo karibu muda wote wa safari yako. Unapoanza safari kutoka kituo kimoja kwenda kingine unashauriwa uwe na walau lita 3 za maji ya kunywa karibu nawe. Ndio sababu ya kubeba mabegi ya migongoni ambapo moja ya bidhaa zilizokuwemo ndani ni maji ya kunywa. Kutokunywa maji ya kutosha si tu kunaweza kukufanya ukashindwa kufika mbali lakini unaweza ukapata madhara makubwa ya kiafya.

Marangu gate to Mandara hut
Hapa ni eneo lijulikanalo kama Kisambionyi au Nusu Njia. Ni eneo ambalo ni nusu ya safari ya kutoka Marangu gate kwenda Mandara Hut. Na ni moja ya maeneo ambako njia ya kupandia wageni na njia ya wabeba mizigo (huku wanaitwa WAGUMU) zinakutana. Daraja hili linaunganisha njia hizi mbili na pia hapa kuna sehemu ya kulia chakula kwa wageni waliobeba vyakula vyao. Pia kuna sehemu ya kujisaidia.

Marangu gate to Mandara hut

Marangu gate to Mandara hut
Safari inaendelea; Vilima kama hivi vinachosha balaa.. unaweza ukatamani ubebwe.

Marangu gate to Mandara hut
Tulianza safari mida ya saa tisa mchana, kutokana na vituo kadhaa na kusimama hapa na pale hatua ya mwisho ya safari yetu kuelekea Mandara Hut ilikuwa ni baada ya jua kuzama. Tuliongozwa na mbalamwezi ambayo ilikuwa inatoa mwanga mzuri mida hii. Tuliingia Mandara hut mida ya saa moja na robo usiku. Hapa tukiwa bado kwenye kichaka karibu kabisa na kufika Mandara hut.

No comments:

Post a Comment