Tuesday, February 26, 2013

Ulindi na Ulimbombo, Wahadzabe bado wanaitumia nji hii mpaka kesho

 Ni ile namna ya kuwasha moto ambayo ilitumika na watu waliopata kuishi miaka na karne kibao zilizopita, Wahadzabe bado wanaitumia njia hii mpaka kesho kama inavyoonekana kwenye picha hizi ambazo mdau Thomas wa HSK Safaris alizipiga kwenye mapori yao maeneo ya Ziwa Eyasi. Picha ya juu ni vijana walioongoza na wageni wa Thom wakionyesha namna wanavyoweza kupata nishati ya moto wanapokuwa porini.

Hapa zoezi limeshakamilika na moto umewaka kama unavyoonekana katikati ya hao vijana.

Wageni wakipata maelezo ya shughuli nzima toka kwa guide aliyeambatana nao. Wahadzabe wanaoishi huku hawajui lugha nyingine zaidi ya lugha yao ile inayofanana na ya Bushmen (Khoisan) wa kule Kusini mwa Africa. Guide ndio wanakuwa wanaifahamu lugha hii na kwa hapa huwa ni wakalimani kati ya wageni na wenyeji. Kwa siku hii Guide aliyeongozana (Aliyeshimama kati na kushika upinde) nao alikuwa ni mtu toka kabila la Datooga (au wengine wamewazoea kuwaita Wamang'ati) ambao nao wanaishi maeneo hayo hayo pembezoni ya ziwa Eyasi. Kama ambavyo mazingira ya picha yanvyojieleza, Wahadzabe wanaishi maporini na huko ndiko wanakopata mahitaji yao ya kila siku aidha kwa uwindaji au kuokoteza. Shukran ya picha kwa Mdau Thomas wa HSK safaris.

No comments:

Post a Comment