Hizi overland truck huwa na vifaa muhimu ambavyo mtu anayeenda kufanya camping. Kuanzia mahema ya kulalia, Viti, meza na vyombo vya kupikia hubebwa kwenye sehemu ya mizigo na hutumika pale vinapohitajika. Overland trucks ni namna nafuu sana ya kufanya safari kwani hubeba watu wengi kwa pamoja hivyo kupelekea kupungua kwa gharama za usafiri ambazo mgeni hutozwa - kwa kuwa gharama inagawanywa kwa wageni ambao mnakuwa mpo wengi. hii ya Lakeland Africa ina uwezo wa kubeba wageni 24.
Viti, meza na mahemu unayoyaona hapo campsite vyote tulikuja navyo na viliwekwa kwenye sehemu ya mizigo chini ya gari
Upande huu wa ndinga ndio kulipowekwa magodoro, mahema na bidhaa nyinginezo muhimu
Huku ni kwa suka na msaidizi wake. wao wanawekewa sehemu yao ya kulala endapo wataamua kutokulala kwenye mahema.
Mtungi wa geni ya kupikia hubebwa na pia una nafasi yake maalum ya kuhifadhiwa wakati wa safari. mkiwa safarini mnakuwa mnakula chakula cha moto muda wote kwa kuwa nishati ya kupikia inakuwepo karibu na kwa urahisi.
Chit-Chatting baada ya breakfast tukisubiri muda usonge tuanze safari ya kurudi dar baada ya kukamilisha ratiba.
Wadau wa Lakeland wakirudishia viti na mahema kwenye mifuko yake maalum ya kubebea kabla ya kuihifadhi kwenye sehemu maalum ya mizigo
No comments:
Post a Comment