Thursday, February 14, 2013

Nyumbu wengine wameshazaa na wanasubiri kuanza mzunguko mwingine

Serengeti Migration Tanzania
Baadhi ya Nyumbu jike wameshamiliza moja ya kazi iliyowaleta Ndutu ambayo ni uzazi, kama invyoonekana kwenye picha ya juu, hao ni watoto waliozaliwa siku si nyingi na tayari wana uwezo wa kwenda sambamba na wazazi wao kama Migration itaanza safari kuelekea kaskazini.

Serengeti Migration Tanzania
Nusu saa baada ya mtoto wa Nyumbu akizaliwa anakuwa tayari ana uwezo wa kwenda sambamba na wazazi wake. hii inaweza kumsaidia pia hata kama sharubu au wanyama wengine wala nyama watamzengea basi ataweza kujitetea walau kwa kukimbia na kulifanya zoezi kuwa gumu kidogo kwa sharubu.

No comments:

Post a Comment