Saturday, February 16, 2013

Mdau Thomas aliwaona Pembe akiwa Ngorongoro crater

Ngorongoro crater Rhino
 Pembe ni jina la porini alilopewa Kifaru na hakuna sehemu nyingine kwa hapa Tanzania ambapo unaweza ukamsikia guide wako akilitamka jina hili zaidi ya Ngorongoro crater. Ngorongoro ni moja ya maeneo ya uhifadhi ambako Pembe wanaweza kuonekana kwa urahisi. Hivi karibuni, Mdau Thomas wa HSK Safaris aliweza kuwabaini pembe watatu waliokuwa pamoja muda mfupi tu baada ya kushuka na kuingia crater. Uwepo wao kwa pamoja ulivutia wageni wengi ambao walikuwa na shauku kubwa ya kuwaona. Kwa bahati mbaya Pembe hawa watatu walikuwa mbali kidogo na barabara hali ambayo ilitoa changamoto kidogo kwa Mdau Thomas pale alipotaka kunasa taswira zao.

Ngorongoro crater Rhino
kwenye picha hii pembe ni hao wanyama watatu waliojikusanya pamoja kati kati

Ngorongoro crater Rhino

Ngorongoro crater Rhino

Ngorongoro crater Rhino
 Shukran ya picha hizi kwa mdau Thomas wa HSK Safaris.

No comments:

Post a Comment