Thursday, December 20, 2012

Mahali yalipo maporomoko ya Kalambo

Kalambo Waterfalls Tanzania
Ni kwenye eneo lililozungushiwa kiduara cheusi, hapo ndipo maporomoko ya Kalambo yalipo. Yapo mpakani kabisa kati ya Tanzania na Zambia. Kwa upande wa Tanzania yapo mkoa wa Rukwa, Karibu na Kijiji cha Kasanga ambao upo pembezini ya Ziwa Tanganyika. Sumbawanga ni ndio mji mkubwa ambao maporomoko haya yapo karibu nao. Kasanga ni moja ya vijiji ambavyo meli Kongwe Duniani inayofanya kazi mpaka sasa ya Mv. Liemba husimama. Picha juu nimeipiga kutoka kwenye moja ya Ramani za Tanzania. Unaweza kufuatilia mwenyewe kwenye Google Maps kama inavyoonekana hapa chini japo eneo yaliyopo maporomoko haya halijakuwa tagged sawasawa.

No comments:

Post a Comment