Tuesday, December 11, 2012

KAMBI POPOTE YA CLOUDS TV KUUNGANA NA LAKELAND AFRICA SAFARI YA SIKU 14 ZA

Lakeland & Kambi popote Clouds TV


Kipindi cha Kambi Popote kinachorushwa Clouds Tv kitaungana na Lakeland Africa kwenye safari ya siku 14 za ‘Mtanzania tembelea Tanzania’ amabyo itaanza desemba 14 mwaka huu na kumalizika desemba 27 mwaka huu. 

Mtangazaji wa kipindi hiki Antonio Nugaz ataiongoza timu yake nzima katika safari hii ya kuvutia huku timu yote kwa ujumla ikipata huduma ya tour guide maarufu kutoka Lakeland Africa mwenye uzoefu wa miaka zaidi ya 3o katika sekta ya utalii.

Safari hii itaanzia Dar es Salaam, na kupita katika hifadhi za Sadan, Pangani, Lushoto, Tarangire, Olduvai Gorge, Ziwa Manyara, Ngorongoro Crater, Hifadhi ya Serengeti na itahitimishwa Butiama kwa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Watanzania watakaosafiri na Kampuni ya Lakeland Africa katika safari hii ya siku 14 za ‘Mtanzania tembelea Tanzania’ watapata huduma safi ndani ya lori la kitalii wakiwa safarini ikiwemo kila mtalii kuwa na soketi yake ya kuchajia simu, laptop na kamera.
Pia kila mtalii atakuwa na kabati lake dogo (locker) kwa ajili ya kufungia vitu vyake vya thamani kama vile passport, vitambulisho na kwamba kila mtalii anatakiwa kuja na kufuli lake la kufungia kabati lake.

Mbali na hayo kila mtalii atakuwa na taa yake ya kusomea wakati wa usiku, gari lina tanki la maji lenye ujazo wa lita 500 na kila mtalii atapewa lita 20 kwa siku na kwamba kutakuwa na firiji ya vinywani baridi na vitu vinavyoharibika.

Kwa mawasiliano na Lakeland Africa
+255222-761811
+255784885901
‘Kuwa mtalii ndani ya nchi yako’

No comments:

Post a Comment