Wednesday, October 10, 2012

Mbuyu Mkubwa Picnik Site, Selous GR


Ni Mbuyu ambao unaelezewa kuwa ni mkubwa sana ndani ya pori la akiba la Selous. Eneo linalozungukwa na mbuyu huu hutumika kama sehemu ya wageni kupatia chakula chao cha mchana wakati wa game drive. hii inahusika zaidi kwa wale ambao wanafanya full day game drive. Ni sehemu ya wazi na wanyama, wakubwa na wadogo, wakali na wapole wanakuwa maeneo jirani. Siku hii tulipokuwa  njiani kuelekea kwenye huu Mbuyu tulikutana na simba jike wawili ambao walikuwa karibu na Mbuyu. Walikuwa ni sehemu ya Lake Manze pride (kundi la simba lijulikanalo kama Lake Manze). Mbuyu huu upo jirani na Ziwa Manze.

No comments:

Post a Comment