Monday, September 10, 2012

Asubuhi moja huko Lushoto

Lushoto Tembea Tanzania
Safari ya matembezi yangu ilianzia Mullers Mountain Lodge, nje kidogo ya mji mdogo wa Lushoto. Lengo kuu likiwa ni kutembelea maeneo mbalimbali ya vijiji na vivutio vilivyo karibu na Eneo ilipo Mullers Mountain Lodge. Hitimisho la safari yangu lilikuwa ni kufika kwenye maporomoko ya maji ya mto Mvuezi. Picha juu ni njia ya kuingilia Mullers Mountain lodge. picha niliipiga nikiwa natoka hivyo hotel ya Mullers nimeipa mgongo.

Lushoto Tembea Tanzania
Eneo hili wenyeji waliita viwanja vya Kagera

Lushoto Tembea Tanzania
Muonekano wa vilima vinavyozunguka eneo la uwanja wa Kagera

Lushoto Tembea Tanzania
Kila upande utakaougeuzi shingo yako utakutana na vilima au mabonde ambayo kwa kipindi hicho (desemba) vilikuwa ni vya kijani kila kona.

Lushoto Tembea Tanzania
Sehemu za mabonde kunakuwa na mito na maji ya uhakika ambayo wenyeji wanayatumia vyema kwa kilimo cha mboga mboga na matunda. Wengi wetu tunaoishi mijini tunajua utamu na uzuri wa matunda toka Lushoto.
Lushoto Tembea Tanzania
Bonde hili lilikuwa limesheheni Mboga mboga. Upande mmoja kulikuwa na Cabbage na upande mwingine kulikuwa na Nyanya

Lushoto Tembea Tanzania
Daraja la kuelekea Shule ya Sekondari ya Kifungilo. Mliosoma huko mnalikumbuka?  Niliambiwa kuwa awali lilikuwa likitumika daraja la mbao/Magogo ambalo linaonekana kulia kwa daraja la Sasa. Mzazi mmoja alipomleta mwanae wakati wa mvua aliguswa na hali ilivyokuwa kipindi hicho na akaamua kujenga daraja bora ambalo ndio linatumika mpaka sasa. Tulipofika hapa kwenye Daraja tuliacha kufuata barabara ya magari na kuingia uchochoroni ili tuweze kufika yalipo Maporomoko ya maji.

Lushoto Tembea Tanzania

Lushoto Tembea Tanzania
Wakati mwingine huwa na kuwa na shauku kubwa ya kufikia kivutio flani lakini nikiwa njian wasiwasi unaweza kuanza kuja taratibu. Hii ni njia tuliyoifuata baada ya kuachana na ile kubwa pale kwenye daraja la Kuelekea Shule ya Sekondari ya Kifungilo.Mwenyeji wangu alinitoa wasiwasi na kuniambia ni njia ambayo hutumika na wengi, japo bado nilikuwa natoa macho kila upande.

Lushoto Tembea Tanzania
Mito ni mingi huku milimani mpaka saa nyingine huelewi kama huu ni mto au mfereji.

Lushoto Tembea Tanzania

Lushoto Tembea Tanzania

Lushoto Tembea Tanzania
Eneo hili lina picnic sites kibao ambapo wageni huja na kupumzika siku nzima.

Lushoto Tembea Tanzania
Maporomoko ya maji ktk Mto Mvuezi, Lushoto

Lushoto Tembea Tanzania
f
Lushoto Tembea Tanzania
Ni eneo tulivu na mwanana. Lina kivuli kizuri cha miti na mabwawa ambayo mtu anaweza kuogelea kama hali ya hewa inaruhusu.

Lushoto Tembea Tanzania
Sehemu za pembezoni mwa mto kuna maeneo ambayo mtu huweza kupumzika. Kama unalitafuta jua basi unaweza kukaa juu ya mawe yaliyopo mtoni.

Lushoto Tembea Tanzania
Mullers Mountain lodge ikionekana kwa mbali tokea moja ya vilima vinavyolizunguka eneo ilipo hoteli

Lushoto Tembea Tanzania
Picha zote toka ktk maktaba ya TembeaTz

2 comments:

  1. Muller's Lodge, quite a nice place

    ReplyDelete
  2. lushoto na Tanga kwa ujumla bado ni kijani sana, bila kusahau wilaya ya Muheza, Pangani, Mkinga, mfano maaeneo ya Maramba..saafi sana. Asanteni sana kwa kutusaidia kutembea Tanzania..

    ReplyDelete