Tuesday, July 3, 2012

PrecisionAir yarejesha safari za Arusha; Yabadili muda wa safari za Johanesburg


Precision Air - Shirika la ndege linaloongoza Tanzania leo imerejesha safari zake jijini Arusha kuanzia Julai 1 baada ya kusimamisha safari zake mapema mwaka jana kwa ajili ya kupisha ukarabati wa uwanja wa ndege wa Arusha iliyokuwa inaongezewa lami.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Biashara wa Precision Air Bw. Patrick Ndekana alisema kwamba shirika hilo la inafuraha kubwa kurejea Arusha baada ya ukamilikaji wa ukarabati wa uwanja nambari 27 wa kurukia uwanjani hapo ambayo itaruhusu ndege kubwa zaidi kutua na kuruka.

“Tunapenda kuwataarifu wateja wetu kwamba tutaanza kuruka kwenda Arusha mara tatu mpaka mara nne kwa wiki kuanzia Julai 1. Hizi safari zinatarajia kukomesha usumbufu ambao wateja wetu wa Arusha wamekuwa wakipata kwa kusafiri kwa gari kwenda na kurudi hadi uwanja wa kimataifa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kukamilisha safari zao,” alisema Ndekana.

Kurejea katika soko hili itaimarisha utalii kwa sababu kutakuwa kuna usafiri mrahisi wa kufikia jiji la Arusha ambayo inasifika sana kwa utalii.   Precision Air pia imejidhatiti kutoa mtandao maradufu kwa wateja wake ili kuweza kuwezesha shughuli za kijamii na kiuchumi kwa kuunganisha mikoa yote nchini Tanzania.

“Arusha ni moja ya miji mikubwa nchini Tanzania, ni nyumbani kwa mashirika yakimataifa na sehemu yanoyotokea makongamano makubwa, bila kusahau shughuli za kitalii. Mkoa huu kwahiyo unahitaji huduma ya usafiri wa anga uliobora na ambao tunamiini sisi Precision Air tunaweza kuitoa, kwahiyo tunapenda kuwa ahidi wateja wetu wategemee mambo makubwa kutoka kwetu,” alisema Ndekana.

Uwanja wa ndege wa Arusha imekuwa ikifanyiwa ukarabati kwa zaidi ya mwaka sasa ili kuweza kufanya uwanja mzima kutumika baada ya kuongeza lami. Marekebisho haya sasa yatawezesha ndege kubwa zaidi kutua na kuruka.

Wakati huo huo, Bw. Ndekana pia ametangaza kwamba kuanzia Julai 1 2012, shirika hilo litabadilisha muda wake wa kusafiri kwenda Johannesburg kutoka saa 10 na nusu jioni hadi saa 4 kamili asubuhi ili kuweza kuwapatia wasafiri urahisi wa kuunganisaha safari kwenda kwingine wafikapo nchini Afrika Kusini. 

Pamoja na mabadiliko hayo, shirika hilo la ndege pia itaanza kutoa huduma ya kuunganisha safari kutokea Johannesburg kwenda Kilimanjaro na Zanzibar kupitia Dar es Salaam ili kuweza kuwapatia urahisi watalii. Hii itafanyika mara 4 kwa wiki ambayo inamaanisha safari za Zanzibar na Kilimanjaro zitaanza kuhudumiwa na ndege aina ya Boeing, wakati ATR zikiendelea pia.
Ukiondoa Arusha, Precision Air pia inasafiri kitaifa kwenda Mwanza, Bukoba, Musoma, Kigoma, Kilimanjaro, Zanzibar, Mtwara na Dar es Salaam. Kimataifa Precision Air inasafiri kwenda Lusaka, Lubumbashi, Johannesburg, Hahaya, Nairobi, Entebbe na Mombasa. 

No comments:

Post a Comment