Thursday, June 28, 2012

Muonekano wa Runway ya JKNIA wakati wa kutua


Wengi wetu tunaziogopa sana hizi ndege ndogo za abiria, lakini ni ndege ambazo zinaweza kumpa abiria undani wa shughuli za rubani awapo ardhini au hata angani. Hii ni kutokana na ndege hizi kuwa katika muundo ambao hauna kizuizi kati ya abiria na rubani. Hivi majuzi tukiwa njiani kurudi Dar kutoka Zanzibar, Kamera ya Tembea Tanzania blog ilipata fursa ya kukaa siti ya mbele sambamba na rubani. Mengi yaliweza kung'amuliwa lakini mtundiko huu unakuletea taswira kadhaa za muonekano wa barabara kurukia na kutua ndege ya uwanja wa ndege wa JKNIA, DSM.

Siku hii tulikuwa tunatua kutokea upande wa Vingunguti.

Boeing ya Precision ikiwa pembeni kutupisha sisi tutue ile na yenyewe iweze kuendelea na mchakato wake wa kuruka. Kwenye usafiri wa anga usalama ni jambo la msingi ambalo halina cha mkubwa wala mdogo. Mambo yanaenda kadri taratibu zinavyoelekeza.1 comment:

  1. Kazi yenu nzuri saana, endeleeni hivyo kuitangaza Tz na vivutio vyake.
    www.ruvumapress.blogspot.com

    ReplyDelete