Tuesday, June 26, 2012

Mpaka wa Selous GR na kijiji cha Mloka


Hapa ni kwenye mpaka kati ya pori la akiba la Selous na Kijiji cha Mloka huko Rufiji. Mgeni anayeingia Selous kwa barabara na kuingia kwa kutumia geti la Mtemere ni lazima apite hapo. Picha hii ilipigwa mida ya jioni na mwelekeo wetu ulikuwa ni kutoka kwenye eneo la hifadhi kurudi campsite tuliyokuwa tumefikia karibu na kijiji cha Mloka. 
Barabara unayoiona pembezoni ni barabara maalum kwa ajili ya wahifadhi kufanya ukaguzi wa mipaka sambamba na kuweka alama ya mpaka baina ya kijiji na hifadhi. Picha imetoka maktaba ya Tembea Tanzania blog, ilipigwa Oktoba 2011

No comments:

Post a Comment