Tuesday, June 26, 2012

Hot Air Balloon juu ya Bwawa la viboko la Seronera - Serengeti NP

Narudia tena, endapo utapata fursa ya kutembelea Hifadhi ya taifa ya Serengeti, wasiliana na muandaaji wa safari yako ili kuangalia uwezekano wa kufanya Hot Air balloon safari ndani ya Serengeti. Japo sasa hivi huduma za haya mapulizo zipo Tarangire pia. Hutajutia wala kusikitika kwani ina mvuto wa kipekee na kukupa muonekano wa Uwanda wa Serengeti kwa namna ambayo hutaitegemea. Hizi ni picha zikionyesha moja ya sehemu ya safari ya Balloon ndani ya Serengeti, hapa likivuka bwawa la Viboko lililopo ktk mto Seronera, maeneo ya Seronera ndani ya Hifadhi ya taifa ya Serengeti.


 Ni bwawa lenye idadi ya viboko wa kutosha

Baadhi ya viboko walianza kuhamaki pale balloon liliposogelea bwawa lao.Njia na mapito unayoyaona nje ya bwawa ni mapito ya wanyama wanaokuja kunywa maji au njia za viboko wanapotoka na kurudi bwawani. Picha toka maktaba ya Tembea Tanzania Blog

No comments:

Post a Comment