Wednesday, May 16, 2012

Tanzania yazidi kufanya vyema kwenye Maonesho ya kimataifa ya utalii ya INDABA huko Durban


Naibu Waziri wa Utalii wa Afrika Kusini Bibi Tokozile Xasa (watatu kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mwendeshaji Biashara na viwanda wa Afrika Kusini Bibi Elizabeth Thabethe  (wa kwanza kushoto) katika picha ya pamoja na baadhi ya waoneshaji kutoka Tanzania wakiongozwa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Dk. Aloyce Nzuki (wan ne kushoto) alipotembelea Banda la Tanzania katika maonesho ya INDABA mjini Durban Afrika Kusini.


Geofrey Tengeneza, Durban.
Banda la Tanzania katika maonyesho ya Utalii ya Kimataifa ya INDABA yanayoendelea jijini Durban Afrika Kusini limeendelea kuvutia viongozi na watu wa kada mbalimbali kutoka ndani na nje ya Afrika Kusini wanaotembelea maonyesho hayo.  Miongoni mwa waliotembelea banda hilo shindwa kuzuia hisia zao hususan kwa maelezo na vielelezo vinavyoonesha uzuri na upekee wa  vivutio vya utalii vya Tanzania na shughuli za utalii zinavyoendeshwa nchini ni Naibu Waziri wa Utalii wa Afrika Kusini Bibi Tokozile Xasa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Viwanda na Biashara la Afrika Kusini Bibi Elizabeth Thabethe  ambao kwa pamoja walitembelea Banda la Tanzania na kujionea vielelezo mbalimbali sambamba na kupata maelezo yaliyowafurahisha sana kuhusu utalii wa Tanzania kwa ujumla.

Akizungumza na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Dk Aloyce Nzuki na waoneshaji wa Tanzania kwa ujumla  Naibu huyo waziri alifurahishwa na kuvutiwa na jinsi Tanzania kupitia Bodi ya Utalii ilivyojipanga katika kuitangaza Tanzania duniani  na jinsi ambavyo Tanzania imekuwa ni mshiriki mzuri wa maonesho ya INDABA na kukiri kuwa Tanzania imekuwa ikitoa changamoto kubwa kwa nchi nyingine wanachama wa SADC katika sekta ya Utalii. “Tanzania ni nchi tishio katika sekta ya utalii miongoni mwa nchi za SADC, ni nchi inayonivutia sana “ alisema Bibi Tokozile Xasa

Jumla ya makampuni 49 kutoka sekta binafsi na taasisi sita za serikali zinashiriki katika maonesho hayo ambayo ni makubwa kuliko yote barani Afrika. Maonesho haya hufanyika kila mwaka jijini Durban Afrika Kusini. Katika maonesho kama haya mwaka jana Banda laTanzania lilitunukiwa tuzo ya kuwa Banda Bora kuliko yote katika maonesho hayo miongoni mwa nchi za SADC.

No comments:

Post a Comment