Wednesday, April 25, 2012

Balloon Safari ndani Ya hifadhi ya Serengeti


Hii ni video ambayo inaweza kukupa mtiririko mzima wa safari ya Balloon ndani ya Hifadhi ya taifa ya Serengeti sambamba na ile staftahi ya porini - Bush breakfast. Ni video iliyopigwa na kuandaliwa na mmoja wa wageni walioitembelea hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kufanya safari ya Balloon mwaka 2009.

Video kama hizi zipo kedekede kwenye youtube na cha msingi ni kujua key-words zitakazoweza kuziibua. Ukitumia Serengeti balloon Safari utazipata kedekede na utapata mwanga wa jinsi safari hizi zinavyoanza mpaka mwisho. Mathalan kweny hii video utaona jinsi abiria wanavyokaa kwenye kikapu kabla safari haijaanza. Huo mkao hutumika wakati wa kuruka na hata wakati wa kutua pia. Kelele utakazosikia ni burners za balloon ambapo hapo rubani wa pulizo anakuwa anachoma hewa iliyopo(baridi) ili ipate joto na kuliwezesha pulizo kukaa hewani bila wasiwasi. Bofya hiyo video ujionee mambo zaidi ambayo nchi yetu imejaaliwa.

3 comments:

  1. imetulia saana hii mazee! inasikitisha kuona wageni ndo wanafaidi haya mambo halafu sie wenyeji tunang'aa macho tunakuwa ignorant of our own environment! thumbs up for this article KK!
    Shime wadau haya mambo ni kujipanga tuu!
    dnyaki

    ReplyDelete
  2. this great adventure at wonderful place thanks for sharing Judi Online
    Jual Rumah
    Mobil Bekas
    Bali Land

    ReplyDelete
  3. cool place, this very wonderful wilds live you can see elephant, zebra ect regards
    Judi Online
    Jual Rumah
    Mobil Bekas
    Bali Land

    ReplyDelete