Thursday, April 12, 2012

Arusha mpaka Namanga

Wiki iliyopita nilikuwa njiani kuelekea kwa watani zetu wa jadi kupitia mpaka wa Namanga. Mtundiko huu una baadhi ya taswira nilizoweza kuzinasa nikiwa njiani. Zote ni za maeneo kuanzia nje kidogo ya jiji la Arusha kuelekea Namanga.

Hapa ni maeneo ya Longido njiani kuelekea Namanga


Kwa wazoefu wa barabara ya Arusha Namanga watakuwa wanaijua vyema hii Savanah. ni Sehemu ambayo mandhari yake inashabihiana na hifadhi ya taifa ya Serengeti - ule uwanda wa nyasi.hali ya barabara kati ya Arusha mpaka Namanga ni nzuri na lami imekamilika. japo sehemu chache ndio kuna marekebisho madogo madogo ya culverts ambazo zitamlazimu dereva kutumia njia ya pembeni. licha ya hivyo, diversion nazo zimeandaliwa vyema.

No comments:

Post a Comment