Wednesday, March 21, 2012

Uko tayari kupanda Bodaboda inayoendeshwa na mwanamama?

Mdau Sam Diah wa Tanzania Travel huko Arusha ameturushia picha hii aliyoipiga leo mchana maeneo ya Sanawari Arusha ambapo kulikuwa na bodaboda mbili ambazo zilikuwa zinaendeshwa na akina mama. Kwa Mujibu wa Mdau Sam ni kwamba sasa hivi fani ya kuendesha bodaboda mkoani arusha imeanza kupata watendaji akina mama ambao nao wanakula vichwa sambamba na machalii wa kiume. Wewe kama abiria, upo tayari kupanda bodaboda inayoendeshwa na mwanamama? Kaa ukijua Arusha na Moshi bodaboda hujulikana zaidi kama Toyo.

2 comments:

 1. Wadau huku Arusha mambo ndiyo hayo. hakuna kazi za wavulana peke yake wadada nao sasa wanaendesha TOYO na kwa kasi ya ajabu.
  Kwa utafiti wa haraka wateja na washabiki wakubwa wa TOYO Arusha na nadhani inaweza kuwa tanzania yote ni kina mama na kina dada. sijui kuna siri gani katika TOYO nawaachia wadau.jioni njema.ahsante sana KK

  ReplyDelete
  Replies
  1. naamini TOYO ikiendesha na mwanamama atakuwa makini zaidi, so ajali zitapungua sana.

   Delete