Wednesday, March 7, 2012

Moja ya raha za kisiwa cha Mbudya

Ni uwepo wa fukwe ambazo inakuwa na maji ya kina kirefu muda wote - maji kupwa au maji kujaa. Hii ni tofauti sana na hali ilivyo huku kwetu na hata kwenye visiwa vingine. Kisiwa cha mbudya kipo kwenye eneo ambalo muda wowote ule wa siku, mgeni anakuwa na uhakika wa kuogelea kadri uwezo wake unavyomruhusu. Huna haja ya kwenda mbali na kuwa ktk hatari ya kuzingirwa na maji kama yatarudi bila ya wewe kubaini mapema.

Sehemu kubwa ya pwani za kisiwa hiki zina mchanga mweupe na safi kwa kutembea. Hata ndani ay maji mchanga upo na kupunguza uoga kwa wale ambao huwa wanatishwa na uwepo wa majini mengi kwenye sakafu ya bahari.

Hali ilivyokuwa upande wa mjini wakati tukienda kupanda boti kwenda Kisiwani. Kilikuwa ni kipindi ambacho maji yalikuwa yamekupwa na kupelekea sisi kulazimika kutembea umbali kuifuata boti ilipokuwa. Kwa Mbudya (muda huo huo) hali ilikuwa ni tofauti kama inavyoonekana katika taswira mbili za juu. Kwa kawaida (maji yakijaa) eneo hili linakuwa na kina cha kutosha tu.

2 comments:

  1. NAOMBA UWE UNA TAJA SEHEMU ILAHISISHE HATA KWA MGENI KUJUA NI WAPI NCHI IPI BY www.eliabu.blogspot.com

    ReplyDelete
  2. Mdau,
    Kisiwa cha Mbudya kipo kwenye Pwani ya Dar Es Salaam maeneo ya Kunduchi. Ukifiatilia vyema kwenye moja ya posts utapata taarifa hizi.

    ReplyDelete