Tuesday, January 10, 2012

Maporomoko ya Maji ya Mto Mvuezi, Lushoto

Ni Maporomoko ya maji ambayo yapo karibu na Shule ya wasichana ya Kifungilo, Wilayani Lushoto mkoani Tanga. Nilifika hapa kwa miguu tokea Mullers Lodge safari ambayo ilituchukua muda wa kama saa moja na robo. Sehemu kubwa ya safari ya kuja hapa iliingiliwa na vituo vya hapa na pale yote ikiwa ni katika kujifunza na kuona mengi mengineyo kuhusu milima ya Usambara na eneo la Lushoto. Kimsingi safari ya miguu ilikuwa na lengo la kunifikisha yalipo haya maporomoko.
Ni sehemu maridhawa kwa mgeni kuja kupumzika na kuweza kupata chakula cha mchana au asubuhi pembezoni mwa mto na maporomoko haya. mahali hapa pana utulivu wa hali ya juu. Kama hali ya hewa inaruhusu mgeni anaweza kuogelea kwenye sehemu mbele ya hapo maporomoko ya maji. kwani swimming pool asilia.


Kama uliwahi kucheza kikapu au long jump unaweza fika kwenye majabali ambayo yapo ndani ya mto wenyewe. Jambo hili lifanywe kwa uangalifu mkubwa kwani uwezekano wa mtu kuteleza na kuumia ni mkubwa pia - mambo ya parking at owners risk.
Mpango mzima wa kufika hapa unaweza kuandaliwa na hoteli uliyofikia na pia unaweza kuja ktk maporomoko haya kwa gari japo utalazimika kuliacha mita kadhaa kabla ya kufika yalipo maporomoko haya. Hii ilikuwa ni mwanzoni mwa mwezi Disemba 2011.

4 comments:

  1. Mh KK ulifikaje hapo kwenye jiwe maana naona kiatu na socks ziko fresh, kwa kuruka naona umbali ni mkubwa.

    ReplyDelete
  2. Anony wa kwanza, shaka ondoa. Kulikuwa na jiwe lingine upande wa kushoto (halionekani kwenye taswira) ambalo ndio lilinisogeza karibu na hapo nilipo kaa.

    ReplyDelete
  3. Kabla hujasema kuna jiwe kulia kwako, nilipiga hesabu kuwa pengine uliruka toka jiwe lililoko kushoto kwako, ila nikawa najiuliza, si panateleza sana hapo na huo uoto wa kijani? si ungevunja meno kwa kuangukia sura na kuondoka na manundu ya kutosha? teh teh, afadhali umetoa jibu.

    ReplyDelete