Monday, December 12, 2011

Wanamuita Drogba..... Mloka, Selous

Kushoto, Ni Mjasiriamali anayefanya shughuli za kupeleka wageni safari za matembezi pembezoni mwa pori la akiba la Selous maeneo yaliyopo ktk kijiji cha Mloka. Yeye safari zake hujulikana kama bush walk ambapo wageni wake hupata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu maisha ya mwanakijiji na wanyamapori. Vitu kama dawa mbalimbali za asili, hadithi za kale huwa ni sehemu ya vitu wanavyojifunza wageni wa 'Drogba'. Zana zake za kazi zimeandika Mwananyika, lakini wanakijiji na mashabiki wake wakaamua kumuita Drogba kutokana na kile kinachoelezewa kuwa wajihi wake unafanana na yule mwanasoka maarufu duniani.

Yeye haingii ndani ya pori la Selous bali hufanyia safari nje ya pori ambako nako pia kunakuwa na wanyama kama tembo, Digidigi, swala na wakati mwingine Nyati pia. Siku hii tulikutana Hippo camp ambayo yeye alikuwa amerudi toka kwenye bush walk na wageni wake. Anapokuwa kazini (kwenye bush walk) huwa anaimba nyimbo mbalimbali za asili ikiwa ni burudani kwa wageni. Kwa sababu za kiusalama, huwa anakuwa anaambatana na askari mwenye silaha.

Zana mbalimbali za jadi ambazo tumeshika ni zana ambazo Drogba huzibeba anakuwa mzigoni. Kamba, ngao, kijembe kidogo, Mkuki na kikapu za asili ni baadhi ya vitu alivyokuwa amebeba alipokuwa kwenye bush siku hii.

2 comments:

  1. kwa macho yangu anafanana zaidi na Michael Essien kuliko Drogba.

    labda kama kuna sifa nyingine, lakini kwa mwonekano huyu ni Essien.

    ReplyDelete
  2. Duu, kweli kazi ni kazi!

    ReplyDelete