Game Walking Safari ni moja ya shughuli ambayo binafsi hupenda kuifanya (pale mazingira yanaporuhusu) ninapoitembelea Hifadhi au pori la akiba. Hivi karibuni nilipata fursa ya kufanya activity hii nilipokuwa pori la akiba la Selous. Kwa kawaida matembezi haya hufanyika mida ya asubuhi au jioni na huchukua muda usiozidi saa moja.
Ni namna nzuri ya kuweza kuyaelewa kwa undani mazingira na maisha ya wanyama wa porini tena kwa ukaribu usio na kifani. Picha zinazoonekana ktk mtundiko huu tulizipiga wakati tukianza safari yetu ktk geti la Mtemere, Selous. Toka kushoto ni Ranger, Mimi, Bavon na mwisho ni Guide wa walking - kumradhi, majina kamili ya ranger na guide yamenitoka.

Ki-utaratibu, game walking safari lazima kuwe na ranger mwenye silaha kwa ajili ya usalama wa wageni. kwani kuna uwezekano mkubwa wa kukutana na wanyama hatari ambao wanaweza kutaka kuleta vurumai. Silaha huwepo kwa lengo kubwa la kutoa onyo kwa mnyama atakayeonyesha azma ya kuleta vurumai. Mara nyingi kwa kupiga risasi hewani na sio kumlenga mnyama husika. Uamuzi wa kumpiga mnyama mwenyewe huwa ni wa mwisho kabisa ambapo ikionekana mnyama hatishiki na warning shots. Guide kazi yake kubwa ni kutoa maelezo ya mambo mbalimbali ambayo mnakutana nayo mkiwa kwenye matembezi au yale ambayo mgeni atapenda kuyaelewa. Ni namn moja nzuri ya kuzielewa hifadhi zetu na hazina zilizomo ndani yake. Unapokuwa kwenye gari mambo mengi huyaoni au unayapita bila kuyaelewa vyema.
No comments:
Post a Comment